Makatazo ya biashara baada ya adhaana ya pili ya ijumaa

Swali: Hanaabilah (Rahimahumu Allaah) wamesema kuwa makatazo ya kufanya biashara siku ya ijumaa baada ya adhaana ya pili yanamuhusu yule ambaye analazimika kuhudhuria swalah ya ijumaa. Inafaa kununua kutoka kwa mwanamke ambaye anauza nje ya mlango wa msikiti?

Jibu: Swalah ya ijumaa inakulazimu wewe. Haifai kwako kununua kitu. Unatakiwa kuiendea swalah. Swalah ya ijumaa inakulazimu wewe, mwanamke haimlazimu. Lakini hata hivyo hapana neno ikiwa mnunuaji ni mwanamke mwenzie au msafiri ambaye haimlazimu swalah ya ijumaa. Lakini hiyo haina maana kwamba maduka yafunguliwe kwa madai kwamba ni kwa wale ambao haiwalazimu swalah ya ijumaa. Hicho ni kitu kisichojuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 13/04/2021