Makafiri pekee ndio watakaa Motoni milele

Swali: Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا

“Yeyote atakayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi hakika atapata Moto wa Jahannam hali ya kudumu humo milele.”[1]

Baadhi wanasema kuwa usengenyi na umbea unaingia katika Aayah hii?

Jibu: Aayah hii ni yenye kuenea na ni kwa lengo la makemeo. Ni lazima kuamini kuwa mwenye kufa juu ya Tawhiyd hatodumishwa Motoni milele ikiwa ataingia. Yuko chini ya matakwa ya Allaah. Baadhi ya Maandiko yanafasiri mengine. Ni kama ambavo kuna baadhi ya Maandiko yanasema kuwa mzinzi na muuaji watadumishwa Motoni milele. Hata hivyo wakiingia sio kuwekwa Motoni maisha yote. Kuna matarajio kwao kutoka na kuingia Peponi. Makafiri pekee ndio wataowekwa Motoni milele.

Swali: Kwa Aayah hii ni kwa njia ya kuogopesha na kuonya?

Jibu. Ni kwa njia ya kuogopesha, kuonya na makemeo.

[1] 72:23

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23251/معنى-الوعيد-في-اية-الجن-لمن-عصى-الله
  • Imechapishwa: 14/12/2023