Swali: Kuna maneno tunayosikia ya kwamba asli kwa majini ni kusema uongo. Je, maneno haya ni sahihi?

Jibu: Hapana, si sahihi. Majini kuna wema na waovu. Si wote wenye kusema uongo.

وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ

“Miongoni mwetu [wako walio] wema na miongoni mwetu [wako walio] kinyume chake.” (72:11)

وَأَنَّا مِنَّا الْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا الْقَاسِطُونَ

“Miongoni mwetu [wako walio] Waislamu na miongoni mwetu [wako walio] wanaopotoa haki” (72:14)

Wao ni kama binaadamu. Si wote wanasema uongo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-15.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020