Swali: Majanga yanayoufika ulimwengu wa Kiislamu ni kwa sababu ya madhambi ya viumbe?

Jibu: Bila ya shaka. Mwenye kuwa na mashaka juu ya hili hana imani. Mwenye kuwekea shaka juu ya kwamba yale yanayoufika ulimwengu ni kwa sababu ya madhambi na kufuru, hana imani:

وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ

“Haukusibuni katika msiba wowote ule, basi ni kwa sababu ya yale yaliyochuma mikono yenu.” (42:30)

Haya mi Maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):

وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ

“Haukusibuni katika msiba wowote ule, basi ni kwa sababu ya yale yaliyochuma mikono yenu.”

ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

“Ufisadi umedhihiri katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale iliyochuma mikono ya watu ili awaonjeshe baadhi ya ambayo wameyatenda ili wapate kurejea.” (30:41)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-8.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020