Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuswali baadhi ya swalah nje ya wakati wake kwa hoja ya kwamba amelala?

Jibu: Ikiwa amelala kwa bahati mbaya na hakukusudia kulala, bali usingizi umempitikia, ni mwenye kupewa udhuru.

“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu aina tatu…”

Mmoja katika hawa ni mwenye kulala mpaka atapoamka.

“Mwenye kusahau swalah au akapitikiwa na usingizi, basi na aiswali pale atapokumbuka.”

Ama ikiwa anakusudia kulala na kusema nitaswali pale nitapoamka, haijuzu kwake kufanya hivi akachelewesha swalah kwa kukusudia na kusema wacha nilale.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-8.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020