Swali: Mtu akifa na akaingia kaburini anamuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Je, huambiwa tunayoyasema juu ya mtu huyu ilihali katika wakati mmoja kunaweza kufa watu wengi? Malaika wawili wanapomuhoji wanamuhoji kwa lugha yake au kwa kiarabu au kwa lugha ya kisirya?

Jibu: Anapofariki mtu na kuzikwa hujiwa na Malaika wawili ambao wanamuuliza juu ya Mola Wake, Mtume wake na dini yake kwa lugha anayoifahamu. Muumini huthibitishwa kuyajibu tofauti na kafiri. Haijalishi kitu hata wakakufa maiti wengi kwa wakati mmoja. Sio jambo la kushangaza. Malaika wana uwezo wasiokuwa nao viumbe.

Kutokana na tunavyojua haikuthibiti kuwa maiti anamuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye kaburi lake.

Tunakuusia urejee katika kitabu “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” cha Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, “al-Usuwl ath-Thalaathah” cha Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab kuhusiana na mada hii na vitabu vinginevyo kwa ajili ya faida zaidi.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (324-325/03)
  • Imechapishwa: 22/08/2020