Swali: Kuna kijana ameuasi akizikwa azikwe na Qur-aan. Ni ipi hukumu ya wasia huu?
Jibu: Asizikwe na Qur-aan. Usitekelezwi sampuli ya wasia kama huu. Haijuzu kuutekeleza. Haijuzu kuzika Qur-aan na maiti. Usitekelezwi kwa kuwa ni kuisaliti Qur-aan na ni Bid´ah. Hakuna kinachomnufaisha mwanaadamu isipokuwa matendo yake. Haijalishi kitu hata kama atazikwa na misahafu mia hakuna kitachomnufaisha isipokuwa matendo yake aloyafanya. Ikiwa alitenda kwa mujibu wa Qur-aan atapata malipo ya kheri na neema kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) hata kama hatozikwa na Qur-aan. Ikiwa ametenda maovu hata kama atazikwa na Qur-aan haitomnufaisha kitu.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-3-14.mp3
- Imechapishwa: 19/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket