Mahali imamu anatakiwa kuswali Sunnah akimaliza faradhi

Swali: Ni daraja ya Hadiyth inayosema:

“Haifai imamu kuswali sehemu ileile aliposwali swalah ya faradhi”?

Jibu: Ninakumbuka kuwa Hadiyth hiyo ni dhaifu. Hilo ndilo ninakumbuka. Nitairejea ijumaa ijayo kwa uhakika zaidi – Allaah akiitaka.

Swali: Je, maamuma akishafanya Adhkaar inazingatiwa kuwa ni maneno na aswali mahali pake?

Jibu: Kwa kuzingatia kwamba Hadiyth ni dhaifu na hilo ndilo lenye kuonekana wazi, basi kilicho bora ni imamu kutoendelea kuswali mahali pale aliposwali swalah ya faradhi. Sababu ni kwamba akibaki hapo, watu wanaweza kudhani kuwa bado anaswali faradhi au kwamba amekosea na anarudia tena swalah. Huenda pia atasikika akinyanyua sauti kwa Takbiyr au kwa kisomo usiku, kisha watu wakaelewa vibaya kama anaendelea na faradhi. Kwa hiyo akihama kutoka sehemu aliyoswali, hilo ni tahadhari zaidi ili watu wasidhani kuwa bado yuko katika swalah au kuzuia mkanganyiko mwingine.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1218/هل-صح-حديث-لا-يصلي-الامام-في-مكانه-الذي
  • Imechapishwa: 14/06/2026