Swali: Sote tunajua mafikio ya washirikina huko Aakhirah, lakini ni yepi mafikio ya watoto wao wadogo wanapokufa? Je, wanaoshwa na kuvikwa sanda na kuswaliwa swalah ya jeneza?
Jibu: Watoto wa makafiri wanaokufa basi wanazingatiwa na wao ni makafiri ulimwenguni. Wakifa kabla ya ule umri wa kupambanua hawatozikwa wala kuvikwa sanda. Hawatoswaliwa na wala hawatozikwa na waislamu, kwa sababu ni makafiri kama baba zao. Kuhusu Aakhirah, Allaah ndiye mjuzi zaidi nini wangefanya. Maoni sahihi ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) atawapa mtihani; wakimtii basi atawaingiza Peponi na wakikataa atawaingiza Motoni.
Hali kadhalika ndio yanayosemwa juu ya wale watu ambao hawakufikiwa na Mitume na ujumbe; Allaah ndiye anayejua nini wangeliwafanya. Wao pia watajaribiwa na yale anayoyataka Allaah na yale yanayopelekea hekima Yake; wakimtii wataingia Peponi na wakimuasi wataingia Motoni.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/442-443)
- Imechapishwa: 14/06/2026
Swali: Sote tunajua mafikio ya washirikina huko Aakhirah, lakini ni yepi mafikio ya watoto wao wadogo wanapokufa? Je, wanaoshwa na kuvikwa sanda na kuswaliwa swalah ya jeneza?
Jibu: Watoto wa makafiri wanaokufa basi wanazingatiwa na wao ni makafiri ulimwenguni. Wakifa kabla ya ule umri wa kupambanua hawatozikwa wala kuvikwa sanda. Hawatoswaliwa na wala hawatozikwa na waislamu, kwa sababu ni makafiri kama baba zao. Kuhusu Aakhirah, Allaah ndiye mjuzi zaidi nini wangefanya. Maoni sahihi ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) atawapa mtihani; wakimtii basi atawaingiza Peponi na wakikataa atawaingiza Motoni.
Hali kadhalika ndio yanayosemwa juu ya wale watu ambao hawakufikiwa na Mitume na ujumbe; Allaah ndiye anayejua nini wangeliwafanya. Wao pia watajaribiwa na yale anayoyataka Allaah na yale yanayopelekea hekima Yake; wakimtii wataingia Peponi na wakimuasi wataingia Motoni.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/442-443)
Imechapishwa: 14/06/2026
https://firqatunnajia.com/377-ni-wapi-wataingia-watoto-wa-makafiri/