Mahali bora pa kuomba du´aa ndani ya swalah ni katika Sujuud

Swali: Bora mtu aombe du´aa anapokuwa amesjudu?

Jibu: Kama alivosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake anapokuwa amesujudu. Hivyo basi ombeni du´aa kwa wingi.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Imekuja katika Hadiyth nyingine ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ama Rukuu´ mtukuzeni Mola. Ama Sujuud jitahidini katika du´aa kuna matarajio mkubwa mkaitikiwa.”

Ameipokea Muslim pia.

Mwishoni mwa swalah pia ni mahali pa kuomba du´aa. Aidha kati ya Sujuud mbili aseme:

ربي اغفر لي، ربي اغفر لي

 “Mola wangu nisamehe. Mola wangu nisamehe.”

Hapana vibaya akiambatanisha na du´aa ya kuomba msamaha.

Swali: Ni mamoja katika swalah ya faradhi au swalah inayopendeza?

Jibu: Ndio, katika swalah ya faradhi na swalah inayopendeza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23116/ما-افضل-اوقات-الدعاء
  • Imechapishwa: 04/11/2023