Swali: Beti ambazo zinakusanya yale maeneo ambayo inafaa kusengenya?

Jibu: Ni dhahiri:

   الذنب ليس بِغِيبَةٍ في ستةٍ

Usengenyi sio dhambi katika pahali sita

لمُتَظَلِّم، ومُعَرِّف، ومُحَذِّرِ

Mdhulumiwa, anayetambulisha na anayetahadharisha

ولمُظْهِرٍ فِسْقٍ، ومُسْتَفْت،ٍ ومَنْ

Anayedhihirisha ufuska, anayeuliza na

طَلَبَ الإعانةَ في إزالة مُنكرِ

anayeomba msaada katika kuondosha maovu

Hali zote hizi ziko wazi. Anayetambulisha maimamu wamewatambulisha wale waliojeruhiwa. Anayetahadharisha kwa mfano mtu katika Ahl-ul-Bid´ah. Anayedhihirisha ufuska wake. Anayeuliza kama mfano wa mwanamke aliyeuliza:

“Ee Mtume wa Allaah! Hakika Abu Sufyaan ni mwanaume bakhili.”

Alikuwa anauliza. Vilevile anayeomba msaada katika kuondosha maovu mahali fulani.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23510/ما-الحالات-التي-تجوز-فيها-الغيبة
  • Imechapishwa: 03/02/2024