Swali: Anayesema “Mwenye kuhifadhi baadhi ya Aayah na Hadiyth ni wajibu kwake kuwalingania watu” kwa kutumia dalili Hadiyth isemayo:

“Fikisheni kutoka kwangu japokuwa Aayah moja”.

Je, kauli hii ni sahihi au ni lazima kwanza ajifunze elimu ya Kishari´ah kwa sampuli zake kisha ndio…

Jibu: Ndugu! Hata kama atahifadhi Qur-aan nzima na Hadiyth zote na kusibaki kitu lakini hata hivyo akawa hafahamu maana yake, haijuzu kwake kuzifasiri na kuwabainishia nazo watu kwa ujinga. Ndio anaweza kuwafikishia nazo kimaandiko kwa njia ya kuwasomea wakahifadhi. Ama kuwafafanulia na kuwafasiria nayo ilihali hajui kitu, hili halijuzu. Haijuzu kwake kufanya hivi. Kufikisha kuna aina mbili:

1- Kufikisha maandiko.

2- Kufikisha maana.

Aina hii ni ya wanachuoni. Kuhusiana na kufikisha maandiko hili wanaingia pia wale waliohifadhi Qur-aan yote au sehemu yake au Hadiyth. Wawasomee wengine kwa njia ya kuwahifadhisha tu. Haifai kwao kuwafafanulia nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (47) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-5-12.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020