Kufupisha katika safari pasi na kunuia

Swali: Je, kufupisha swalah katika safari kunahitajia nia kabla ya kuingia katika swalah?

Jibu: Msingi kwa msafiri ni kuwa anafupisha. Fuqahaa´ wanasema ni lazima anuie. Lakini hili sio lazima. Ikiwa mazowea yake huwa anafupisha kwa kuwa ana udhuru wa safari, inafaa kwake kufupisha hata kama hakunuia mwanzoni wa swalah yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (47) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-5-12.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020