Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن ابن مسعود رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : ((إنَّهَا سَتَكونُ بَعْدِي أثَرَةٌ وأُمُورٌ تُنْكِرُونَها!)) قَالُوا: يَا رَسُول الله، فَمَّا تَأْمُرُنا؟ قَالَ: ((تُؤَدُّونَ الْحَقَّ الَّذِي عَلَيْكُمْ، وَتَسأَلُونَ الله الَّذِي لَكُمْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

51 – Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika baada yangu kutakuwa na ubinafsi na mambo ambayo mtayapinga.” Wakasema: “Unatuamuru nini?” Akasema: “Mtekeleze haki iliyo juu yenu na nyinyi mumuombe Allaah haki yenu.”

Kuna maafikiano juu yake.

52 – Katika upokezi mwingine imekuja:

فَاصْبِرُوا حَتَّى تَلْقَوني عَلَى الحَوْضِ

“Kuweni na subira mpaka mtapokutana na mimi kwenye Hodhi.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawalekeza kuwa na subira hata kama watadhurika kwa hilo. Kuwa na subira juu ya dhuluma za watawala ni miongoni mwa sababu za kupata hodhi na kunywa maji yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/282)
  • Imechapishwa: 26/04/2023