Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن ابن مسعود رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّهَا سَتَكونُ بَعْدِي أثَرَةٌ وأُمُورٌ تُنْكِرُونَها!)) قَالُوا: يَا رَسُول الله، فَمَّا تَأْمُرُنا؟ قَالَ: ((تُؤَدُّونَ الْحَقَّ الَّذِي عَلَيْكُمْ، وَتَسأَلُونَ الله الَّذِي لَكُمْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

51 – Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika baada yangu kutakuwa na ubinafsi na mambo ambayo mtayapinga.” Wakasema: “Unatuamuru nini?” Akasema: “Mtekeleze haki iliyo juu yenu na nyinyi mumuombe Allaah haki yenu.”

Kuna maafikiano juu yake.

Anachokusudia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwamba waislamu watatawaliwa na watawala ambao watasimamia mali yao na kuitumia kama wanavopenda na kuwanyima waislamu haki zao kwa mali hiyo. Hii ni dhulumu wafanyayo watawala kuitumia mali ambayo waislamu wana haki nayo na badala yake waitumie wao wenyewe dhidi ya waislamu. Wakasema:

“Unatuamuru nini?”

Akasema:

“Mtekeleze haki iliyo juu yenu…”

bi maana kitendo chao kisiwafanyeni mkawanyika haki zao zilizo juu yenu ikiwa ni pamoja na usikivu, utiifu, uasi na vurugu. Bali kinyume chake unachotakiwa ni kusikiliza, kutii, usitake kuangusha uongozi aliyopewa na Allaah.

“… na nyinyi mumuombe Allaah haki yenu.”

bi maana ombeni haki yenu kutoka kwa Allaah. Ikiwa na maana muombeni Allaah awawaongeze ili waweze kutekeleza haki zenu zilizo juu yao. Hii ni katika hekima ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Hakika (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitambua kuwa nyoyo zina vifundo na haziwezi kuwa na subira juu ya mwenye kujiingiza katika haki zao. Ndio  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawa ameelekeza katika jambo ambalo linaweza kuwa na kheri: kutekeleza haki tulizo nazo juu yao, ikiwa ni pamona na kuwasikiliza na kuwatii, kutowafanyia uasi na kadhalika, na sisi tunamuomba Allaah haki yetu. Tukisema:

“Ee Allaah waongoze ili waweze kutupa haki zetu”

Hilo linakuwa na kheri kwa njia mbili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/280-281)
  • Imechapishwa: 26/04/2023