Swali: Je, madhambi yanaongezwa kwa ukubwa au idadi katika maeneo matakatifu kama Haram?

Jibu: Madhambi hayaongezwi kwa idadi, isipokuwa kwa njia ya namna. Dhambi moja linalipwa mara moja. Allaah (´Azza wa Jall):

وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ

”Na atakayekuja na ovu, basi hatolipwa isipokuwa mfano wake; nao hawatodhulumiwa.”[1]

Lakini dhambi inayofanywa katika maeneo matakatifu ni khatari zaidi; nakusudia kwa upande wa dhambi yenyewe na si idadi. Haiongezwi; haiwi kumi na kadhalika. Hata hivyo ni khatari. Madhambi yanayofanywa Haram, Madiynah, Shaam au wakati wa Ramadhaan ni kubwa zaidi kwa uzito wa dhambi. Hata hivyo haiongezwi. Kila dhambi moja inalipwa mara moja. Isitoshe madhambi yanatofautiana kwa upande wa namna – ukubwa wa dhambi yenyewe.

[1] 06:160

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24979/ما-كيفية-مضاعفة-السيىات-في-البلد-الحرام
  • Imechapishwa: 17/01/2025