Fidia ya anayemuua njiwa na ndege Haram

Swali: Ni ipi hukumu ya anayekata mti?

Jibu: Anapaswa kumwomba Allaah msamaha na kutubu Kwake. Ikiwa atatoa swadaqah, basi basi Allaah atamlipa kheri na ni jambo zuri. Inasimuliwa kutoka kwa Ibn ´Abbaas na wengine kwamba kwa mti mkubwa kuna fidia ya kuchinja ngamia, kwa mti mdogo ni kondoo na kwa majani ni thamani yake. Ikiwa mtu atafanya hivyo kwa ajili ya kuchukua tahadhari, basi ni jambo zuri.

Swali: Vipi kuhusu kuua njiwa au ndege wadogo kama shomoro ni halali?

Jibu: Haijuzu, kwani wote wanachukuliwa kuwa wanyama wa kuwinda.

Swali: Fidia yao ni nini?

Jibu: Kwa njiwa, fidia yake ni kondoo ikiwa aliuawa kwa makusudi, na kwa shomoro ni thamani yake.

Swali: Je, kuna Hadiyth sahihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inayozungumzia fidia hii?

Jibu: Sifahamu Hadiyth yoyote kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24974/حكم-قطع-الشجر-وقتل-الحمام-في-الحرم
  • Imechapishwa: 17/01/2025