Je, mtu anatakiwa kugusa nguzo ya yemeni ikiwa hakuigusa?

Swali: Je, mtu ambaye hakuweza kugusa nguzo ya yemeni anatakiwa kuashiria na kusema “Allaahu Akbar”?

Jibu: Aashirie jiwe jeusi peke yake. Haikuthibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliashiria kiguzo cha yemeni. Kwa maana nyingine mtu hatakiwi kuashiria kiguzo cha yemeni. Ni sawa akiweza kuigusa, lakini ikiwa hawezi anapita tu bila kuashiria. Haikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba aliashiria isipokuwa tu jiwe jeusi.

Swali: Je, mtu anapaswa kusema “Allaahu Akbar” kwenye nguzo ya yemeni?

Jibu: Anasema “Allaahu Akbar” ikiwa ataugusa. Ikiwa hatagusa, anapita tu. at-Twabaraaniy amepokea Hadiyth kwa cheni ya wapokezi nzuri inayosema kwamba:

”Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa alipougusa nguzo ya yemeni husema:

بسم الله، والله أكبر

”Kwa jina la Allaah, Allaah ni Mkubwa.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24984/هل-يشار-للركن-اليماني-اذا-لم-يتيسر-استلامه
  • Imechapishwa: 17/01/2025