Swali: Amri ya kumuua nyoka wakati wa swalah ni kwa njia ya ulazima au ni ya mapendekezo tu?

Jibu: Allaah ndiye ajuaye zaidi. Amri hiyo inaashiria kuwa jambo hilo limewekwa katika Shari´ah. Lakini kusema kuwa la lazima, ni jambo linahitaji kufikiriwa. Hata hivyo inaonyesha kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24978/هل-الامر-بقتل-الحية-في-الصلاة-للوجوب
  • Imechapishwa: 17/01/2025