Swali: Takfiyriyyuun wamewaathiri vijana kwa njia mbaya sana. Wanaitakasa Takfiyr yao kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kuwepo kwa mabenki ya ribaa pamoja na mapenzi kwa wasiokuwa waislamu.
Jibu: Maamuzi ya kuwa na mabenki ya ribaa, haina maana kuwa mtu anaonelea kuwa ni halali. Kuwepo kwa dhambi ni kitu, wakati kuihalalisha ni kitu kingine. Kuwepo kwa dhambi haina maana kuwa mtu anaonelea kuwa ni halali. Kunaweza kupatiakana dhambi wakati huo huo mtu anakubali kosa lake na anajua kuwa anafanya dhambi. Kuhusiana na kuonelea kuwa ni halali, inazingatiwa kwa yule mwenye kusema:
“Ni halali, sio haramu.”
Huku ndio kuonelea kuwa kitu kinajuzu. Hata hivyo haina maana kuwa mtu anahalalisha dhambi hii kwa sababu tu ipo.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kanda ”al-Hamalaat al-I´laaniyyah dhiwdd Hukkaam wa ´Ulamaa’ Bilaad-il-Haramayn”
- Imechapishwa: 05/09/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)