Swali: Yapi maoni yako kuhusu maandamano yanayofanyika katika baadhi ya miji ya Kiislamu? Wasemaje kwa yule ambaye anasema yanaruhusu muda wa kuwa ni ya amani, bila silaha na mambo mengine? Na ipi Radd yako kwa yule ambaye anaita watu katika maandamano nchini Saudi Arabia? Tunataraji kutoka kwako kutufafanulia, kutubainishia na kutupa nasaha?

Jibu: Maandamano ni katika mambo mepya, na kila mambo mpya ni Bid´ah, na kila Bid´ah ni upotofu, na kila upotofu Motoni. Hii, kwa kuwa Shari´ah ya Allaah imekamilika – katika Qur-aan na Sunnah. Na hatujui ya kwamba kuna dalili katika Qur-aan na Sunnah inayoruhusu kundi la watu kutoka nje na kuandamana na kuwaudhi watu na kupoteza muda. Je, kuna upotofu mwingine zaidi kuliko huu, ya kuwa Swalah inawachwa na watu wanakufa. Muislamu mmoja tu kupoteza maisha katika maandamano, anapata dhambi yule alie nyuma [ya maandamano], sawa akiwa ni mtu binafsi au ni kuna kundi. Katika Athariy sahihi:

“Kutokomea kwa dunia nzima ni sahali kwa Allaah kuliko muislamu mwanaume kufa.”

Ni wangapi wanakufa katika maandamano? Hili linatolewa ushuhuda na ripoti, akili, ada, ukweli na ushahidi wa macho.

Haya maandamano ni katika Bid´ah na upotofu. Ni Shaytwaan na watu wa matamanio na wabaya ndio huita (watu katika) kwayo. Hawa maadui hawajumuiki isipokuwa dini na vitu vya kidunia huharibiwa, jambo ambalo linajulikana katika haya maandamano. Matukio yote ya maandamano husababisha mauaji, uharibifu, kupoteza mali na wakati na kukandamiza watu wasiokuwa na hatia. Mambo haya yana madhambi mangapi? Dalili ya kwamba ni hasi, inatosha kujua hayakuwepo wakati wa Mitume na Manabii. Walipewa mitihani na kujaribiwa kutoka kwa watu wao pamoja na waliowaamini walifikwa na hayo. Licha na yote hayo hawakuandamana kamwe. Hawakuwa wakilipua na wala hawakuua. Uislamu umeharamisha yote hayo.

Hawa watu ambao wanaita watu katika maandamano na wanaona kuwa ndio uokovu, amechukua njia potofu. Ni bora kwao kurudi katika haki na kutatua mambo kwa misingi ya Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wa wanachuoni waliobobea katika elimu. Yule ambaye anaita watu na ghasia hizi na anasababisha ufisadi katika ya nchi na watu. Ambayo yanaendelea, na bado yanaendelea mpaka hivi sasa, ni ushahidi wa hilo.

Sisi tunaonya wanafunzi wasishawishiwe na wale ambao wanaoyaruhusu maandamano na kusema kuwa maandamano ya amani yanaruhusu. Wamefanya mgawanyiko huo bila ya dalili yoyote sahihi katika Qur-aan, Sunnah wala matendo ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), Maswahabah wala wanachuoni. Badala yake, ni kama nilivyosema mwanzo, jambo ambalo hata wengine wamesema.

Kwa ufafanuzi kwa yule ambaye anataka kujua haki, inatosha na yale ambayo Kibar-ul-´Ulamaa wameandika. Wamekubaliana ya kwamba maandamano pamoja na njia zake zote zinazotumiwa ni makosa na yanakosa msingi katika dini na kwamba yanachangia ufisadi katika nchi na watu. Haya ni maoni sahihi. Zaidi ya wanachuoni ishirini wameandika kufafanua haya. Kwa kweli, wanachuoni wengine wote maarufu wanafundisha watu ya kwamba maandamano haya ni njia ya uharibifu na sio njia ya mafanikio na kutengeneza. Wanawafundisha mfumo sahihi ni kumnasihi mtawala. Kama amekosea, anasihiwe na abainishiwe kosa lake kivyake. Aitwe katika haki kwa njia iliokuwa nzuri bila ya kusababisha ghasia hizi zinazochangia watu kupoteza maisha yao na watu salama kutiwa khofu na mengine yote ambayo yamejitokeza leo na hapo kabla na Allaah anajua zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=119407
  • Imechapishwa: 05/09/2020