Maandamano ni kujifananisha na makafiri kikamilifu


Haya maandamano… ambayo tulikuwa tukiyaona kwa macho yetu wakati Ufaransa ilipokuwa inatawala Syria, na tulikuwa tukiyasikia katika miji mingine na sasa tumeyasikia [tena] Algeria. Lakini Algeria imezidi miji mingine kwa upotevu huu na kujifananisha huku [na hawa makafiri]. Kwa kuwa tulikuwa hatuoni wasichana pia wanashiriki kutoka nje kwenye maandamano, jambo ambalo kikamilifu ni kujifananisha na makafiri na makafiri wa kike. Kwa sababu ndio tunayoyaona kwenye picha na TV na redio,wanatoka maelfu ya makafiri wakiume na wakike mchanganyiko, sawa ikiwa ni wa Ulaya, Syria au wengine. Wanasongamana wanawake na wanaume na huenda hata sehemu za mbele zikagusana na makalio. Huku ni kujifananisha na makafiri kikamilifu, nako ni kutoka wasichana na wavulana kutoka nje na kuandamana.

Jambo lingine ni kwamba haya maandamano kuna kujifananisha na makafiri wazi wazi kwa kupinga au kuonesha kwao hasira zao kwa baadhi ya kanuni ambazo viongozi wao wamewawekea, nitaongezea kitu kimoja. Haya maandamano ya kiulaya ambayo waislamu wamekuja kuyaiga kichwa mchunga, siyo njia ya Kishari´ah kwa kutengeneza hukumu na kutengeneza jamii.

Kuanzia nukta hii yanakosea makundi na mapote yote ya Kiislamu ambayo hayafuati njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kutengeneza jamii. Jamii haibadilishwi kwa nidhamu za Kiislamu kwa fujo, maneno mabaya na maandamano. Bali [jamii inabadilishwa] kwa utulivu na kueneza elimu kati ya waislamu na kuwalea na Uislamu huu hadi malezi haya yalete matunda, hata kama litapatikana hili baada ya kipindi kirefu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawa Juddah (12)
  • Imechapishwa: 05/09/2020