Swali: al-Faqiyh anaita katika maandamano Saudi Arabia. Ni ipi hukumu ya hili?

Jibu: Maandamano ni jambo sio la Kiislamu. Ni jambo geni kwa waislamu. Haijuzu kwa waislamu kuandamana.

Kuhusu Sa´d al-Faqiyh, al-Mas´ariy, Usaamah bin Laadin na watu mfano wake, ni watu wanaita katika fitina, ufisadi na uharibifu. Haijuzu kwa yeyote kuwaiga au kufanya kama wanavyotamani. Wanachotaka ni kuharibu kati ya Saudi Arabia na wananchi. Ni jambo lisilojuzu. Mwenye kufanya hivo anatenda dhambi.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?feature=youtu.be&v=jnEoorDnTgQ