Hakika sisi tunalingania katika Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hatulinganii katika Sunnah za baba zetu na babu zetu. Na wala hatulinganii katika Sunnah ya Hasan al-Bannaa.

“al-Ikhwaan wana mnara. Kila yaliomo humo ni mazuri. Usiulize nani kaujengea! Ni Hasan al-Bannaa. Mnara wenu ulioharibika uko wapi? Alikuwa ni Suufiy! Mnara wenu ulioharibika uko wapi? Alikuwa ni Suufiy! Kaja na ibara:

“Tutasaidizana kwa yale tunayoafikiana na kusameheana kwa yale tunayokhitilafiana.”
Katu! Katu! Allaah amesema:

وَتَعَاوَنُواْ عَلَى الْبرِّ وَالتَّقْوَى وَلاَ تَعَاوَنُواْ عَلَى الإِثْم وَالْعُدْوَانِ

”Saidianeni katika wema na uchaji Allaah. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

Je, wataka kufuta Shari´ah ya Allaah wewe Hasan al-Bannaa, na ukaifanya kuwa ni matamanio yetu!! Alikuwa ni Ishtiraaq (socialist) pia. Nilisoma katika kitabu chake anasema inatakikana kwa serikali kuchukua mali ya matajiri na kuwapa mafukara na kuwapa matajiri ziada fulani. Porojo tupu! Kwanini asiseme serikali tangu mwanzo iwape mali [… sauti haiko wazi]? Na tangu lini imekuwa inajuzu kwetu kuchukua mali kwa matajiri na kumpa fakiri? Na Allaah amesema katika Kitabu Chake:

وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ

”Ole wao hao wapunjao!” (83:01)

Adhabu inawangoja wale wenye kupunja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuchukua shibri ya ardhi kwa dhuluma, Allaah atamwacha aende mpaka kwenye ardhi ya saba.”

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

انظُرْ كَيْفَ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَى بَعْضٍ وَلَلآخِرَةُ أَكْبَرُ دَرَجَاتٍ وَأَكْبَرُ تَفْضِيلاً

”Angalia vipi tulivyowafadhili baadhi yao kuliko wenginewe. Na hakika Aakhirah ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi.” (17:21)

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَاللّهُ فَضَّلَ بَعْضَكُمْ عَلَى بَعْضٍ فِي الْرِّزْقِ

”Na Allaah amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki.” (16:71)

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَةَ رَبِّكَ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُم مَّعِيشَتَهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِيَتَّخِذَ بَعْضُهُم بَعْضًا سُخْرِيًّا وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ

”Kwani wao ndio wanaogawa rehema za Mola Wako? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wenginewe wawatumikie. Na rehema za Allaah ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya.” (43:32)

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/sounds.php?sound_id=33
  • Imechapishwa: 20/07/2020