Ama usulubu ambao umezoeleka leo. Kusema kuwa fulani ni:

“Salafiyyah katika ´Aqiydah na Ikhwaaniyyah katika mfumo”

Huu ni usulubu na istilahi chafu, potofu na yenye kutatiza. Ni nini maana ya mfumo wa Ikhwaaniyyah? Ni ipi mfumo wa al-Ikhwaan [al-Muslimuun]? Mfumo wa al-Ikhwaan [al-Muslimuun] wao wenyewe hawawezi kubainisha mfumo wao. Shaykh Hasan al-Bannaa (Rahimahu Allaah), anaisifu Da´wah yake ya kwamba ni Suufiyyah, Salafiyyah au Ash´ariy. Anaisifu kwa migongano. Hivyo sisi wenyewe hatutajua mfumo mmoja apitayo juu yake. Kwa ajili hiyo, watu hawa wenyewe hawajui mfumo wao. Mfumo wao unaweza kutofautiana kutokea mji hadi mwingine, na hili analijua yule ambaye kaishi katika miji mbalimbali. Utawaona kuwa ni wenye kutofautiana, na huenda wakawa katika mji mmoja. Utaona wana mfumo wa kutofautiana, kila kikundi kina mfumo wake. Kwa sababu ni mfumo potofu. Msizitaabishe nasfi zenu. Huyu kijana amewasomea Bid´ah mpya [ya kusema fulani ni Salafiy Ikhwaaniy] enyi vijana. Ni juu yenu kubakia juu ya haki. Nyinyi mko katika haki na mtaendelea kuwa katika haki – Allaah akitaka.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.eljame.com/mktba/catplay.php?catsmktba=3
  • Imechapishwa: 20/07/2020