Maana ya Mtume kulishwa na Allaah anapokuwa amefunga

Swali: ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuunganisha swawm. Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Hakika wewe unafunga kwa kuunganisha.” Akasema: “Mimi si kama nyinyi. Mimi hulala nikilishwa na kunyweshwa na Mola wangu.”

Ameipokea pia Abu Hurayrah, ´Aaishah na Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anhum).

Jibu: Ni chakula maalum. Ni yale anayomfungulia Allaah katika nyenzo za maliwazo na kupata ladha ya kunong´onezwa naye. Sio chakula kinachofahamika. Angelikuwa ni mwenye kula basi asingefunga. Ni yale ambayo Allaah anamfungulia moyoni mwake katika maliwazo ya kumtaja Allaah na kumtii ndio yanachukua nafasi ya chakula.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22109/معنى-حديث-ابيت-عند-ربي-يطعمني
  • Imechapishwa: 27/10/2022