Swali: Tunaomba mtuwekee wazi ni nini Bid´ah na aina zake?

Jibu: Bid´ah ni ´ibaadah ambazo hazikuweka Allaah. Kama mfano wa kusherehekea maulidi, usikuwa Israa´ na Mi´raaj, muadhini kunyanyua sauti kwa kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kumaliza kutoa adhaana na mfano wa hayo. Kuna wanachuoni waliotunga vitabu kuhusu Bid´ah na aina zake. Tutaelekeza katika baadhi yavyo:

1 – Kitaab-us-Sunan wal-Mubtada´aat cha Shaykh Muhammad Ahmad ´Abdis-Salaam al-Hawaamidiy.

2 – Kitaab-ul-Ibdaa´ fiy Madhwaar-il-Ibtida´aah cha Shaykh ´Aliy al-Mahfuudhw.

Vyote viwili ni vya wanachuoni wa Misri. Kabla yavyo kwa muda mrefu kuliandikwa kitabu “al-Bid´ah wan-Nahiy ´anhaa” cha Imaam Muhammad bin al-Wadhdhwaah na kitabu “al-I´tiswaam” cha ash-Shaatwibiy.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/327)
  • Imechapishwa: 23/08/2020