Kusherehekea siku ya 27 Ramadhaan

Swali: Ni ipi hukumu ya kusherehekea usiku wa ishirini na saba Ramadhaan peke yake?

Jibu: Kusherehekea usiku wa ishirini na saba peke yake ni Bid´ah iliyozushwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayezusha katika dini yetu hii yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Kilichowekwa katika Shari´ah ni kuuhuisha [usiku huo] kwa ´ibaadah, swadaqah na kadhalika kama masiku kumi mengineyo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/41)
  • Imechapishwa: 23/08/2020