Swali: Nina ndugu yangu ambaye tumekuja naye katika ´Umrah ambaye anasema kuwa mwenye kumtukana Swahabah sio kafiri. Unamnasihi nini? Ni ipi hukumu ya wale ambao wanawatukana Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hawatukani Maswahabah wa Mtume isipokuwa ni kwa sababu ana uadui na Uislamu. Maswahabah wa Mtume wamefanya nini mpaka awatukane? Walifanya propaganda juu ya kuinusuru dini hii, kusuhubiana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupigana Jihaad, kueneza elimu na kulingania katika dini ya Allaah. Ni kwa nini anawatukana? Anawatukana kwa sababu ya kheri walioifanya, Jihaad, kulingania katika dini ya Allaah na kusuhubiana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Hakuna yeyote ambaye ana imani moyoni mwake anawatukana. Hakuna anayewatukana isipokuwa ni adui wa Uislamu na waislamu. Isitoshe mtu huyu anamkadhibisha Allaah (´Azza wa Jall) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu Allaah amewasifu Maswahabah; Muhaajiruun na Answaar kisha huyu anawatukana. Allaah anawasifu na wewe unawatukana? Hii ina maana anapingana na Allaah (´Azza wa Jall). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwatukane Maswahabah zangu.”

Wewe unawatukana Maswahabah! Je, unamuasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Baada ya hapo utadai kuwa wewe ni muumini? Hili ni kosa kubwa. Huku ni kupingana na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je, kutabaki imani pamoja na kupingana na Allaah na Mtume Wake? Hakubaki imani yoyote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13958
  • Imechapishwa: 24/06/2020