al-Fawzaan kuhusu ujinga ni udhuru 10

Swali: Wale wanaoyaomba uokozi makaburi, wanayachinjia na kuweka nadhiri kwa ajili yake bila ya kujua hukumu za Kishari´ah wanapewa udhuru kwa kutokujua?

Jibu: Ndugu! Watu hawa wanasikia Qur-aan:

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا

“Mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote.” (04:36)

Allaah amekataza shirki. Maana ya shirki ni kuabudu asiyekuwa Allaah miongoni mwa makaburi, makuba na vinginevyo. Wanasoma Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.” (04:48)

لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ

“Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni al-Masiyh mwana wa Maryam.” Na al-Masiyh alisema: “Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Mola wangu na Mola wenu. Kwani hakika yeyote atakayemshirikisha Allaah bila shaka Allaah atamharamishia Pepo na makazi yake yatakuwa ni Motoni – na madhalimu hawatopata mwenye kunusuru yeyote.” (05:72)

Wanasoma na kuzisikia Aayah hizi, ni kwa nini basi wasiulize maana ya shirki ili waweze kujiepusha nayo? Ama kusema kuwa ni mjinga, mpaka lini ataendelea kuwa mjinga ilihali Qur-aan inasomwa, anaisikia na yeye mwenyewe anasoma Qur-aan na ni muislamu. Ni kwa nini basi?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13407
  • Imechapishwa: 24/06/2020