Kuswali swalah zote wakati mtu anapoamka

Swali: Una nasaha yoyote kuwapa vijana ambao wanakesha usiku na wanalala wakati wa Fajr na wakati wa ´Aswr kwa hoja ya usingizi?

Jibu: Usingizi sio hoja katika hali hii. Usingizu ukikushinda baadhi ya nyakati unakuwa na udhuru. Ama kuchukulia kuwa ndio ada unalala na kusema nitaswali pale nitapoamka, hii sio hoja. Mtu huyu hana swalah. Lau ataswali hana swalah yoyote.

Enyi waja wa Allaah! Mcheni Allaah enyi. Ziswalini swalah kwa nyakati zake. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا

“Hakika swalah kwa waumini ni faradhi iliyowekwa nyakati maalum.” (04:103)

Bi maana zimefaradhishwa katika wakati ambao Allaah na Mtume Wake wameubainisha. Hivyo haijuzu kucheza na swalah na mtu akaziswali zote katika wakati mmoja. Hili halijuzu. Isitoshe hata akiziswali hazisihi kwa kuwa sio swalah ambazo Allaah na Mtume Wake wameamrisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13958
  • Imechapishwa: 24/06/2020