Lini unamalizika muda wa kuchinja ´Iyd-ul-Adhwhaa?

Swali: Lini unaisha wakati wa kuchinja kichinjwa cha ´Iyd-ul-Adhwhaa?

Jibu: Wakati wake unaisha kwa kuzama kwa jua katika siku ya nne. Ukimchinja dakika kadhaa kabla ya kuzama kwa jua basi anazingatiwa ni kichinjwa cha ´Iyd-ul-Adhwhaa. Hata kama utammaliza baada ya hapo [jua kuzama] hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (25/94)
  • Imechapishwa: 25/07/2020