Swali: Kama unavojua hii leo vitabu na tungo zimekuwa nyingi juu ya maudhui yote. Je, unaweza ukatupendekezea vitabu muhimu zaidi katika maudhui yote kwa mwanafunzi?

Jibu: Mosi mimi sikuzizunguka fani zote na wala sikuzunguka kila kilichoandikwa katika maudhui fulani. Mambo yakishakuwa hivo, basi Allaah haikalifishi nafsi zaidi ya uwezo wake.

Hata hivyo natoa nasaha za jumla. Lazimianeni na vitabu vya wale wa kale.  Vitabu vya wale waliotangulia. Ni vyenye baraka zaidi. Ni vyenye umairi zaidi. Vimetokamana na imani. Pamoja na hivyo hawakukingwa na makosa.

Kwa mtazamo wangu vitabu vingi vya watu wa leo ni vya juujuu. Ndani yake hakuna elimu iliyoingia kwa kina zaidi. Ukileta kitabu cha daktari wa juu kabisa kidaraja basi utaona kuwa ni kitupu. Watu hawa ni wa kijuujuu. Mengi wanayoandika ni nukuu na pengine nukuu zenyewe hazijathibitishwa au pengine hata zimekengeushwa kutoka katika msingi. Kwa sababu hawana elimu ya maana nyingi. Matokeo yake wananakili tu na kuchanganya mambo. Kwa hivyo nasaha zangu kwa wanafunzi wote ni kwamba walazimiane na vitabu vya wale wa kale. Ni vyenye baraka zaidi. Ni wachache wa kujikakama. Ni wenye kuzungumza machache. Watunzi wengi wa leo wanaweza kuandika kurasa mbili juu ya kitu fulani na hakuna unachojifunza isipokuwa misitari miwili pekee. Lakini vitabu vya wale waliotangulia ndani yake mna baraka kwa sababu hawakuwa wenye kujikakama. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Wameangamia wenye kuchupa mpaka.”

Wakati fulani unaweza kupata namna ambavo kijitabu cha udaktari kina kursa kumi juu ya hoja za maoni pande mbili ilihali wale wanachuoni wa kale, kama mfano wa mtunzi wa ”al-Mughniy” na ”Sharh al-Muhadhdhab”, anahitajia juu ya hilo kurasa mbili peke yake. Kwa ajili hiyo nawanasihi ndugu zangu wanafunzi watilie bidii vitabu vya wale waliotangulia.

Swali: Tuchague kitabu kipi cha Fiqh?

Jibu: Kitabu kama “al-Mughniy” cha Ibn Qudaamah na ”Sharh al-Muhadhdhab” cha an-Nawawiy. Hivi ndivo ninavyovijua. Huenda vipo vitabu vyengine nisivyovijua.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (211 B) Tarehe: 1420-03-17/1999-07-01
  • Imechapishwa: 16/01/2021