Lazima kwa mume kumgharamia mkewe Hajj?

Swali: Je, mume analazimika kumgharamia mke wake hajj baada ya kuwa na uwezo?

Jibu: Hajalazimishwa. Hajj inamlazimu yeye ikiwa ana uwezo mwenyewe. Ama mume wake halazimishwi. Ikiwa mke hana uwezo, hajj si wajibu kwake. Tusemeje ni jukumu la mume kwa sababu tu anao uwezo? Hapana, si jukumu lake. Lakini akimfanyia wema na kumgharamia hajj, hili ni jambo la wema na maadili mema. Vinginevyo si wajibu kwake, bali ni wajibu kwake mwanamke ikiwa ataweza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25145/هل-يلزم-الزوج-المستطيع-حج-زوجته
  • Imechapishwa: 07/02/2025