La lufanya imamu anapozidisha Rak´ah

Swali: Maamuma afanye nini ikiwa imamu atazidisha Rak´ah ya tano? Je, akae na kusubiri mpaka pale imamu atapotoa salamu na yeye atoe salamu pamoja nao?

Jibu: Ni wajibu kwake kumzindua kwa kusema “Subhaan Allaah”. Ikiwa hakurejea na wakati huo huo maamuma ana uhakika kuwa amezidisha, asimfuate. Badala yake akae, akipenda atatoa salamu kivyake na akipenda atasubiri na kutoa salamu pamoja nao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (65) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-04-09.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020