Mwanamke kujitoa kwa mwanaume mwema amuoe

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kujitoa mwenyewe kwa mwanaume ambaye anamuona kuwa ni mwema ili aweze kumuoa au hili ni jambo maalum kufanyiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hili ni jambo zuri. Amtumie mtu na kuzungumza naye ikiwa akiridhia dini yake na tabia yake. Mtu huyo anaweza kuwa walii wake au mwanamke mwenzake. Ni sawa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (65) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-04-09.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020