Swali: Wajibu wa wanazuoni ni kusema haki na wasiogope lawama ya mwenye kulaumu kwa ajili ya Allaah. Basi kwa nini matokeo yao hayaonekani ilihali tunaona ufisadi unaongezeka?

Jibu: Wajibu ni kusema haki, lakini si sharti ikubalike. Haki inasemwa na kufafanuliwa. Lakini si kila kinachosemwa huonekana athari zake, wala si lazima akubaliwe msemaji kutokana na sababu nyingi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1034/واجب-العلماء-تجاه-الفساد
  • Imechapishwa: 08/01/2026