Kwanini hukubaki wakaendelea kufaidika nawe?

Swali: Kuna sharti zipi za kuishi kati ya washirikina?

Jibu: Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚقَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا

“Hakika wale ambao Malaika wamewafisha hali wamejidhulumu nafsi zao, wataulizwa: “Mlikuwa katika hali gani?” Watasema: “Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi”, [Malaika] watasema: “Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa pana mkahajiri?” Basi hao makazi yao yatakuwa ni Motoni – na ubaya ulioje mahali pa kurejea! Isipokuwa wale waliokandamizwa – kati ya wanaume na wanawake na watoto – ambao hawakuweza kupata namna yoyote wala hawawezi kuongoza njia.”[1]

Hapana vibaya ikiwa anaweza kudhihirisha dini yake huko na wakati huohuo ana usalama juu ya dini, watoto wake na familia yake. Ingawa mimi naona kuwa hawezi kuwa na usalama juu ya watoto wake kwa sababu analazimika kuwapeleka katika shula za manaswara. Mtoto akikimbia kutoka kwa baba yake anachukuliwa na serikali na hapo baba yake hana tena mamlaka juu yake. Vivyo hivyo juu ya mwanamke. Kwa ajili hiyo mimi naona kuwa haijuzu kuishi katika nchi hizo isipokuwa tu kwa dharurah au mtu ambaye ameenda kulingania kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na wakati huohuo anajiaminisha kutokana na mitihani kama za wanawake na dunia. Nimeambiwa na mmoja ambaye alienda Ubelgiji wakati aliporudi baada ya watu kufaidika naye, nikamuuliza ni kwa nini hakubakia huko kwao ili waendelee kufaidika naye, akajibu kuwa kuna mitihani. Nikamwambia asafiri pamoja na mke wake, akajibu kuwa mitihani sio ya wanawake pekee, bali kuna mitihani ya kidunia na mingine mingi. Kwa hivyo ikiwa anachelea majaribu kwa nafsi yake atalazimika kukimbia na dini yake.

[1] 04:97-98

  • Mhusika: ´Allaamh Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 58-59
  • Imechapishwa: 26/02/2024