Kuzungumzia neema ni katika kuzishukuru neema?

Swali: Je, kunaingia katika kushukuru neema ya kwamba mtu anaizungumzia kama kusema ”Allaah amenineemesha kitu fulani”?

Jibu:

وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ

”Ama kuhusu neema ya Mola wako izungumzie.”[1]

Kuzizungumzia kwa namna ya kuzishukuru ni katika kuzishukuru. Mtu azizungumzie kwa njia ya kutambua neema ya Allaah, na si kwa njia ya majivuno na kiburi.

[1] 93:11

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24681/هل-من-شكر-النعمة-التحدث-بها
  • Imechapishwa: 23/11/2024