Ni ipi hukumu ya anayewakejeli wanaoshikamana na Sunnah?

Swali: Ni ipi hukumu katika zama zetu kwa mtu mwenye kuwakejeli wale wanaoshikamana na Sunnah?

Jibu: Hukmu yake ni kwamba ni dhalimu. Ni wajibu kumtia adabu na kuzuiwa. Ikiwa ishtihzai yake ameikusudia dini anakufuru. Lakini ikiwa istihzai yake anamlenga mtu mwenyewe, kutembea kwake, maneno yake na mfano wa hayo, kitendo hicho kinakuwa haramu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24681/هل-من-شكر-النعمة-التحدث-بها
  • Imechapishwa: 23/11/2024