Swali: Ni lipi jambo limewekwa katika Shari´ah wakati wa kula; kuzungumza au kunyamaza?

Jibu: Lililowekwa katika Shari´ah ni kusema “Bismillaah”. Ama kuhusu kuzungumza ni jambo linaloruhusiwa [mubaah]. Haina neno wakazungumza na ndugu zake na marafiki zake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4740
  • Imechapishwa: 17/11/2014