Wanasema – yaani Jahmiyyah na vijukuu vyao – lau tutasema kuwa (Allaah) anazungumza kwa herufi na sauti tutakuwa tumemfananisha na viumbe kwa kuwa viumbe ndio wanazungumza kwa ulimi na midomo na mifupa ya koo. Vipi wakati mawe na miti vilipozungumza bila ya ulimi na midomo?

Msemo wenu ya kwamba maneno hayawezi kuwepo isipokuwa mpaka kwa herufi na sauti na kwenye mishipa ya koo, yote haya ni uongo. Miti ilizungumza kwa idhini ya Allaah, ipo siku viungo vya mwili vitazungumza na viwatolee ushuhuda wenye navyo, ardhi itazungumza, miamba itazungumza bila ya kuwa na kuwa na koo, midomo na kadhalika. Wao wanamlinganisha Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) na viumbe Wake halafu haya mwisho wake yanawapelekea katika kukanusha Sifa zote za Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/370)
  • Imechapishwa: 19/05/2015