Qur-aan, Tawrat, Injiyl, Zabuur, Suhuf ya Ibraahiym na Muusa (´alayhimaas-Swalaatu was-Salaam) ni katika elimu ya Allaah. Vilevile vitabu vyote ambavyo Allaah ameteremsha kwa Mitume Wake, sawa vile ambavyo vimetufikia na ambavyo havikutufikia, vyote hivo ni katika maneno ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Qur-aan ni katika elimu ya Allaah (´Azza wa Jall). Elimu ya Allaah haiwezi kuwa imeumbwa. Hii ni katika hoja ambayo imewaponda Jahmiyyah. Kwa kuwa Imaam Ahmad – kama itavyokuja huko mbeleni – aliwauliza “Je, elimu ya Allaah imeumbwa?” Wakasema “Hapana”. Hivyo akasema “Basi Qur-aan ni elimu ya Allaah”. Akatumia ushahidi wa Aayah:

وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ

“Na ukifuata matamanio yao baada ya yale ambayo yaliyokujia katika elimu.“ (02:120)

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/342)
  • Imechapishwa: 19/05/2015