Kuzungumza kabla ya kutoa Tasliym ya pili

Swali: Mswalaji akitoa Tasliym moja kisha akazungumza kabla ya Tasliym ya pili. Ni ipi hukumu ya swalah yake?

Jibu: Kuna tofauti kwa wanachuoni. Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa Tasliym moja inatosheleza na Tasliym ya pili ni Sunnah. Wanachuoni wengine wanaonelea Tasliym zote mbili ni wajibu.

Inatakiwa kwa mtu asizungumze mpaka baada ya kutoa Tasliym zote mbili. Hili ndio linalotakikana kwake. Lakini akishatoa Tasliym moja swalah yake ni sahihi kwa mujibu wa wanachuoni wengi. Japokuwa baadhi ya wanachuoni wanaonelea kuwa sio sahihi. Hata hivyo inatakiwa kwa mtu kwa hali yoyote asizungumze isipokuwa mpaka baada ya kutoa Tasliym mbili. Hata baada ya kutoa Tasliym mbili haitakikani kwake kuzungumza isipokuwa kwa yale yaliyothibiti katika Sunnah. Atendee kazi Sunnah. Baada ya kutoa salamu aseme “AstaghfiruAllaah, AstaghfiruAllaah, AstaghfiruAllaah” mara tatu, kisha aseme “Allaahumma antas-Salaam, wa minkas-Salaam, Tabaarakta dhal Jalaal wal-Ikraam”. Ikiwa ni imamu awageukie maamuma kwa uso wake na kusema “laa ilaaha illa Allaah, wahdahu laa shariyka lah, lahul mulku walahul hamdu wa huwa ´alaa kulli sha-in qadiyr” na akipenda anaweza kuzidisha “wa huwa yuhyiy wa yumiyt”. Halafu aseme “laa ilaaha illa Allaah, wa laa na´abudu illaa iyyaah, laa hawla wa laa quwwata illa billaah, laa ilaaha illa Allaah wa laa na´abudu illaa iyyaah, lahun-ni´imatu wa lahul-fadhwl, wa lahuu ath-Thanaau husnaa, laa ilaaha illa Allaah, mukhliswiyna lahud-Diyna walau karihal kaafiruun. Allaahumma laa maniy´ limaa A´twaita, wa laa mu´twiya limaa maana´ta, wa laa yanfau´ dhal jaddu minkal jaddu”. Aseme haya. Kisha baada ya hapo ndio anaweza akazungumza. Haya ndio yanayompasa Muislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4740
  • Imechapishwa: 01/05/2015