Kuswali nyuma ya imamu usiyejua kuwa anajua al-Faatihah

Muulizaji: Ikiwa humjui mtu huyu (kama hajui al-Faatihah) na ukaswali nyuma yake kisha akamalizia swalah yake kwa Suurah hii…

Jibu: Ikiwa humjui msingi ni usalama, msingi mchukulie kuwa anajua al-Faatihah. Huu ndio msingi. Baada ya hapo ukijua kuwa hajui al-Faatihah au anabadilisha maana yake, irudi swalah yako.

Muulizaji: Ina maana inakulazimu kurudi kuswali na maamuma wengine wote?

Jibu: Ndio. Ni lazima kuirudi. Ukihakikisha kuwa imamu hajui al-Faatihah au anasoma kisomo kinachobadilisha maana, ni lazima kurudi swalah kwa kuwa amefanya kasoro katika nguzo miongoni mwa nguzo za swalah. Ama ikiwa hujui msingi ni usalama.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4740
  • Imechapishwa: 01/05/2015