Kuzingatia pesa uliyokopesha kuwa ni zakaah baada ya kushindwa mkopeshwaji kuilipa

Swali: Baadhi ya watu wanamkopa mtu mkopo akashindwa mkopeshwaji kurudisha wanazingatia mkopo huo kuwa ametoa zakaah.

Jibu: Hapana, deni haliwi zakaah. Ni lazima amsubiri. Atapozishika mkononi atazitoa kama zakaah. Vinginevyo amsaidie kwa pesa isiyokuwa zakaah. Haina neno kama amemwachia nazo kama swadaqah. Kuhusu zakaah haitolewi kutoka kwenye pesa ya deni. Pesa ya zakaah anatakiwa kutoa kile alichonacho. Kuhusu deni amsubiri na ampe muda. Ni mwenye kushukuriwa na mwenye kulipwa thawabu iwapo atamsamehe kwa ajili ya kutafuta radhi za Allaah na asizingatie kuwa ametoa zakaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22951/حكم-مدين-يطلب-من-داىنه-اعتبارها-زكاة
  • Imechapishwa: 21/09/2023