Swali 25: Hayo yalitokea mwaka gani? Kipi kilichotokea mwaka huo?

Jibu: Hayo yalitokea mwaka wa kumi baada ya kuwa kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwaka huohuo akafariki mke wake Khadiyjah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na ami yake Abu Twaalib. Mwaka huohuo ndio (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisoma Suurah ”an-Najm” ambapo yeye akasujudu na waumini na washirikina nao wakasujudu naye. Wakati waislamu Wahajiri wa Uhabeshi walipofikiwa na khabari hiyo baadhi yao wakarejea Makkah wakifikiria kuwa Quraysh wamesilimu. Lakini kwa masikitiko mambo hayakuwa hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 99
  • Imechapishwa: 21/09/2023