Kuweka Qur-aan au vitabu vya elimu kama Sutrah

Swali: Je, inajuzu kuchukua Qur-aan Tukufu na kuifanya kuwa Sutrah yangu au baadhi ya vitabu vya elimu?

Jibu: Ama kuhusu Qur-aan bora zaidi iwe mahali pa juu, ambapo haiwi katika hali ya kudharauliwa. Hivyo basi ikiwa mtu ataweka mbele yake baadhi ya vitabu vya elimu, kwa sababu hana Sutrah nyingine, basi dhahiri ni kuwa sijui kama kuna ubaya wowote juu ya jambo hilo. Ikiwa mahali ni safi, basi hakuna ubaya wowote. Kuhusu Msahafu, ni jambo la kutafakari kwa undani zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27369/هل-يجوز-جعل-المصحف-سترة-للمصلي
  • Imechapishwa: 10/04/2025