Swali: Ni ipi hukumu ya kumuuzia mshirikina nguo ya hariri?

Jibu: Maoni sahihi kwa mtazamo wangu ni kwamba haijuzu. Asisaidie katika batili. Imepokelewa kwamba ´Umar alikuwa akiwatumia hariri baadhi ya jamaa zake katika makafiri. Lakini pengine alikuwa akifanya hivo ili zivaliwe na wake zao.

Swali: Haifahamishi kuwa inafaa?

Jibu: Hapana, haiko wazi. Pengine alikusudia zivaliwe na wake zao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23294/حكم-بيع-ثوب-الحرير-الى-الرجل-المشرك
  • Imechapishwa: 22/12/2023