Swali: Je, watoto wa washirikina wanaswaliwa pindi wanapokufa?

Jibu: Hapana. Ulimwenguni wana hukumu moja kama familia zao. Hawaswaliwi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wao ni katika wao.”

Hawaswaliwi ulimwenguni. Wakiuliwa wana hukumu moja kama wao ulimwenguni. Ninachokusudia ni kwamba zikiuliwa familia zao au wakafa watoto wao wanawafuata familia yao. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Wao ni katika wao.”

Hapa ni kuhusu hukumu za duniani. Lakini kuhusu hukumu za Aakhirah  wataokoka ikiwa hawakufikiwa [na ujumbe].

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23392/هل-يصلى-على-من-مات-من-اولاد-المشركين
  • Imechapishwa: 09/01/2024